Site Loader

Dibaji

Mnamo mwaka 1991 madaktari waliopata shauku ya tiba za milimani walimuona mkwea mlima makini akifa katika mlima wa Mera La.Tabibu aliyekuwa naye hakuwa na maarifa mengi juu ya magonjwa ya milimani.

Tanzia hii iliwashajiisha madaktari kujifunza magonjwa ya kiuwanda wa juu na kuwapa wengine taarifa hii.Taasisi iitwayo TIBA-DHARURA  ‘Medical expedition’ ikazaliwa kwa hili kama jukumu lake.

Miaka kumi baadaye,tena katika mlima wa Mera La,wanachama wa tiba-dharura maarufu kama medical expeditions walimuona bi-kizee  wa kijapani akizimia kisha kuaga dunia kwa kuachwa nyuma na rafiki yake.Roho nyingine ilipotezwa licha ya tafiti zote na elimu yote.Kuna mengi yanayohitajika kuokoa roho kama hizi.

Tangu mwanzoni mwa miaka ya tisini(1990) wanachama wa tiba-dharura,’Medical expedition’ pamoja na wengine wamekuwa wakifanya tafiti za tiba za milimani.

Wamejitahidi kuboresha maarifa ya madaktari husika au washauri wa wasafiri wa nyanda za juu

Kitabu hiki kimekitwa kwenye namna taathira za usafiri wa nyanda za juu zinavyoweza kuudhuru mwili wako na shabaha za  kujuza kwa nini ujihisi vibaya au uugue.Hupendekeza mbinu za kuzuia magonjwa na kipi kifanyike ukikabiliwa na magonjwa yanayohusiana na nyanda za juu.

Uzoefu wetu wenyewe na uchunguzi kifani zimejumuishwa.Vifo katika mlima Mere La vilisababishwa na kwenda kwenye uwanda wa juu ingawa vyote vingeweza kuepukwa endapo maelekezo rahisi tu yangezingatiwa.

Tiba-dharura, maarufu kama ‘Medical Expeditions’ huelimisha madaktari kuhusu magonjwa ya nyanda za juu na kuwashajiisha wengine  wayajue pia.Kitabu hiki ni jitihada zetu kuu kumsaidia kila mmoja kuwa salama anaposafiri kwenye nyanda za juu.

Previous         Next