Site Loader

Watoto katika uwanda wa juu

Watoto hukumbwa na matatizo yaleyale ya watu-wazima kwenye uwanda wa juu,japokuwa si rahisi kutabiri ni lini hukumbana nayo.Ni vizuri kukwea polepole kuruhusu watoto kuzoea mabadiliko ya mazingira.

Watoto wadogo hawawezi kueleza namna wanavyohisi.Muongozaji aongozwe na muonekano wa mtoto,kula, kulala na kucheza kwake.Afya ya zote  hizi zikidorora,watoto wamekumbwa na magonjwa ya nyanda za juu na waendelee kuwepo kwenye uwanda huohuo la sivyo,washuke  chini hadi wapatapo nafuu.

Watoto wakubwa huweza kueleza yanayowasibu mlimani kama watu wazima. Elewa hizo ni dalili za magonjwa yasababishwayo na milima na waruhusu wasalie waliko au washuke hadi wapatapo nafuu.

Kwenye uwanda wa juu:
• Matibabu kwa watoto ni sawa nay a watu wazima isipokuwa kwa watoto chini ya kg 40 wapewa dozi ndogo na hupenda dawa za majimaji maarufu kama syrup.
• Uwe na kadi yenye uzito wa motto, dawa zake na dozi.
• Kumbuka kushuka ndiyo dawa bora zaidi.

Maandalizi:
• Pata ushauri wa daktari miezi mitatu kabla ya kuondoka.
• Jali mavazi yako, upatikanaji wa maji safi na salama, losheni ya jua, miwani ya jua ili kuzuia kujisikia hovyo na kujihakikishia malengo halisikaji.
• Andaa namna utakavopata usaidizi mwanao akiugua mlimani au ukiugua wewe mwneyewe.
• Hakikisha ni utalii sahihi kwa watoto.

Tommy, kijana mwenye umri wa miaka minne alipelekwa mapumziko ya kuteleza kwenye barafu katika bonde la Arapahoe Colorado m.3290.Alipenda sana kuwa na rafiki zake bondeni ila alisumbuka sana wakati wa usiku katika siku ya kwanza kwenye eneo la pumziko.Siku iliyofuata iliyofuata hali ilikuwa mbaya Zaidi na kushindwa kula.Baada ya hapo alipelekwa kwa daktari wa hotelini na akapendekeza ashushwe baada ya kugundua ana dalili za magonjwa ya milimani. Kwenye bonde alipata nafuu baada ya masaa sita.

Previous         Next