Site Loader

Peo

Kwenye uwanda wa juu,uko kwenye hatari ya kuungua na kukakamaa mwili.Kiwango kikubwa cha miale ya UV huweza kusababisha kirahisi kubabuka .Oksijeni ndogo na kanieneo la kiwango cha chini husababisha ngozi yako kuwa na ugonjwa wa kuganda tishu kwa jalidi.Hasa watu wenye tatizo la mzungu stahiki wa damu.(Kama ugonjwa wa ‘Raynaud’)

Ugonjwa wa jalidi huweza kutokea kokote kule mwilini kwenye hali ya hewa ya jotoridi la mgando au kwenye kimbunga.Dalili za awali ugonjwa wa jalidi ni uwepo, ganzi na ugumu wa ngozi.Kujipa joto kunakuwa na uchungu sana na ngozi hugeuka nyekunde, huwasha, yenye madoa na iliyovimba.Kuganda kukiendelea, malengelenge huweza kutokea na mwisho ngozi hugeuka nyeusi na kufa.Hii ni hatari kwani huweza kusababisha kukatwa kwa miguu na mikono.

Sehemu nyingi za mwili zi hatarini kuungua jua na athari za baridi ziko kwenye zile za nje-midomo, vidole, pua, masikio.Kwa hiyo, viungo hivyo huhitaji uangalizi maalum.

Uvimbe mkononi, usoni na kifundoni kwenye miinuko ni kawaida.Si jambo la hatari ingawa huweza kuhitaji kukaguliwa na daktari kwa magonjwa mengine.

Kwenye uwanda wa juu:
• Hakikisha mikono na miguu inakuwa mikavu muda wote. Badili glovu na soksi zilizolowa haraka.
• Vaa nguo zinazotosha vizuri.
• Tumia losheni za jua.
• Jifunike dhidi ya jua, baridi na upepo..

Maandalizi:
• Uwe na losheni za jua (SPF 15-30).
• Jizuie kabisa dhidi ya jua.
• Uwe na glovu, soksi, kofia na buti. Hakikisha vinakutosha.

Wakati wa poromoko la theluji la milima ya Himalaya, watu tisa walipoteza maisha na wengine wengi walijeruhiwa.Majeruwalichukuliwa kwa ndege kwenda hospitalini.wachukuzi waliachwa kujirusha wenyewe nyumbani.Baadhi yao walipoteza maisha njiani kwa baridi. Mavazi waliyovaa hayakuweza kuwasitiri dhidi ya baridi na hawakuthubutu kutoa chochote kwenye mabegi waliyobeba.Walifia jirani na mabegi yenye mavazi ya joto milimani.

Previous         Next