Site Loader

Moyo/Damu

Kuzuru kwenye uwanda wa juu kuna madhara mengi kwenye moyo.Oksijeni ya kiwango cha chini kwenye hewa na zoezi unalofanya huweza kuufanya moyo wako udunde kwa kasi.Hili si tatizo isipokuwa kama una matatizo ya moyo (mf.shambulizi la moyo) huweza kutia mshikemshike usio wa kawaida kwenye moyo.shinikizo lako la damu huweza kupanda kidogo kwenye uwanda wa juu, ingawa taathira hii si rahisi kuonekana.

Moja ya taathira ya uwanda wa juu ni kwako wewe kuzalisha Zaidi seli nyekundu za damu (Ili uweze kusheheneza oksijeni ya kutosha kwenye damu) hii inaweza kufanya damu iwe nzito,na kusababisha mzunguko wa damu kuwa wa taratibu.Ukizingatia hili ni vema ukanywa vya kutosha.Kama una tatizo la moyo(kama mdundo wa moyo usio sawia,shinikizo la moyo,shambulizi la moyo au angina) au umekuwa na upasuaji wa moyo ni lazima umueleze daktari wako unachotarajia kufanya  ili usilete usumbufu usio wa lazima  kwenye moyo.Ukimeza dawa,hakikisha unakuwa na maji ya kutosha upandapo..

Ukiwa na afya njema kusafiri kuelekea uwanda wa juu hautaleta shida moyoni mwako kuliko kufanya mazoezi makali katika mwambao wa pwani.

Watu wenye sikoseli ya kurithi wako hatarini na wasiende kwenye nyanda za juu.

Kwenye uwanda wa juu:
• Tembea taratibu, usindane.
• Pumzika vya kutosha.
• Kunywa majimaji mengi.
• Utakapokumbana na tatizo la magonjwa ya nyanda za juu, ishia hapo usiendelee
• Dalili zikiendelea, shuka chini.

Maandalizi:
• Uwe na siha njema.
• Jaribu mazoezi nyubani kabla ya kwenye uwanda wa juu.
• Hakikisha una dawa zote/ maelekezo ya daktari.

Kwenye ziara ya Medex,presha yangu ilirekodiwa ikiwa 168/118 siku moja.Mmoja wa madaktari alisema lilikuwa jambo la kawaida katika kupanda juu lakini hujirekebisha yenyewe mwili uzoeapo kutumia oksijeni kidogo.Alinishauri kwamba siku yangu ya pumziko ni vema kutumika kirahisi,hata kama nilijisikia vizuri.

Previous         Next